Related items
Showing items related by metadata.
-
Book (stand-alone)
-
Brochure, flyer, fact-sheet
-
Book (stand-alone)Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu Kwa Muktadha wa Uhakika wa Chakula na Kuondoa Umaskini 2019Mwongozo wa hiari wa kuhakikisha uvuvi mdogo unakuwa endelevu; katika muktadha wa uhakika wa chakula na kuondoa umaskini umeandaliwa kama nyongeza ya Taratibu za Kimaadili za Uvuvi zinazozingatia uwajibikaji, ambazo ziliandaliwa chini ya uratibu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) mwaka 1995 (Code of Conduct for Responsible Fisheries CCFRF) na kukubaliwa nchi nyingi duniani. Aidha, Mwongozo huu wa hiari ni mahsusi kwa ajili ya kuangaza na kuweka taratibu zinazuhusu uvuvi mdogo. Sababu kuu iliyopelekea kuandaa Mwongozo maalumu kwa ajili ya uvuvi mdogo ni kwamba; kwa kiwango kikubwa jamii ya wavuvi wadogo imeendelea kuachwa nyuma, na umaskini katika jamii hizi umekuwa ni wa kiwango kikubwa. Hali hii ya kusikitisha inatokea wakati ambapo uvuvi mdogo huchangia nusu ya samaki wote wanaovuliwa duniani, na huajiri asilimia 90 ya wavuvi na wafanyakazi wengine katika Sekta ya Uvuvi duniani. Hivyo, imeonekana kuna umuhimu mkubwa wa kuandaa Mwongozo huu, ili kuangazia changamoto mbalimbali zinazowakabili wavuvi wadogo, na kubainisha mbinu ambazo zinaweza kutumiwa katika kutatua changamoto hizo. Mwongozo unabainisha masuala yote muhimu katika mfumo mzima wa mnyororo wa thamani ikiwa ni pamoja na usimamizi wa rasilimali ya uvuvi, masuala ya maendeleo ya jamii ya wavuvi wadogo, thamani ya mazao na biashara, pamoja na umuhimu wa kujenga mazingira bora yanayoimarisha shughuli za uvuvi mdogo kwa kuzingatia masuala ya jinsia na Haki za binadamu.
Users also downloaded
Showing related downloaded files
No results found.