Thumbnail Image

Mwongozo Wa Hiari Kuhusu Uwajibikaji Katika Usimamizi Wa Umiliki Wa Ardhi, Maeneo Ya Uvuvi Na Misitu Kwa Ajili Ya Upatikanaji Na Uhakika Wa Chakula Kwa Taifa

FAO. 2021. Mwongozo Wa Hiari Kuhusu Uwajibikaji Katika Usimamizi Wa Umiliki Wa Ardhi, Maeneo Ya Uvuvi Na Misitu Kwa Ajili Ya Upatikanaji Na Uhakika Wa Chakula Kwa Taifa. Kenya.Related items

Showing items related by metadata.

 • Thumbnail Image
  Book (stand-alone)
  Mwongozo wa Hiari wa Kuhakikisha Uvuvi Mdogo Unakuwa Endelevu Kwa Muktadha wa Uhakika wa Chakula na Kuondoa Umaskini 2019
  Mwongozo wa hiari wa kuhakikisha uvuvi mdogo unakuwa endelevu; katika muktadha wa uhakika wa chakula na kuondoa umaskini umeandaliwa kama nyongeza ya Taratibu za Kimaadili za Uvuvi zinazozingatia uwajibikaji, ambazo ziliandaliwa chini ya uratibu wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) mwaka 1995 (Code of Conduct for Responsible Fisheries CCFRF) na kukubaliwa nchi nyingi duniani. Aidha, Mwongozo huu wa hiari ni mahsusi kwa ajili ya kuangaza na kuweka taratibu zinazuhusu uvuvi mdogo. Sababu kuu iliyopelekea kuandaa Mwongozo maalumu kwa ajili ya uvuvi mdogo ni kwamba; kwa kiwango kikubwa jamii ya wavuvi wadogo imeendelea kuachwa nyuma, na umaskini katika jamii hizi umekuwa ni wa kiwango kikubwa. Hali hii ya kusikitisha inatokea wakati ambapo uvuvi mdogo huchangia nusu ya samaki wote wanaovuliwa duniani, na huajiri asilimia 90 ya wavuvi na wafanyakazi wengine katika Sekta ya Uvuvi duniani. Hivyo, imeonekana kuna umuhimu mkubwa wa kuandaa Mwongozo huu, ili kuangazia changamoto mbalimbali zinazowakabili wavuvi wadogo, na kubainisha mbinu ambazo zinaweza kutumiwa katika kutatua changamoto hizo. Mwongozo unabainisha masuala yote muhimu katika mfumo mzima wa mnyororo wa thamani ikiwa ni pamoja na usimamizi wa rasilimali ya uvuvi, masuala ya maendeleo ya jamii ya wavuvi wadogo, thamani ya mazao na biashara, pamoja na umuhimu wa kujenga mazingira bora yanayoimarisha shughuli za uvuvi mdogo kwa kuzingatia masuala ya jinsia na Haki za binadamu.
 • Thumbnail Image
  Brochure, flyer, fact-sheet
  Utambuzi wa Sansuli katika Maeneo Wazi ya Samaki wa Bahari ya Hindi 2023
  Kadi hizi za utambulisho hutolewa na Tume ya Tuna ya Bahari ya Hindi (IOTC) kusaidia kuboresha data ya kukamata na takwimu juu ya billfish inayolengwa. Kupitia uelewa bora wa hifadhi za billfish, mameneja wa uvuvi wa kikanda wanaweza kuhakikisha kuwa aina hizi zinavuliwa kwa njia endelevu katika Bahari ya Hindi. Watumiaji wanaowezekana zaidi wa kadi ni waangalizi wa uvuvi, sampuli, na mabwana wa uvuvi. Taasisi za mafunzo ya uvuvi na jumuiya za uvuvi ni watumiaji wengine wenye uwezo.
 • Thumbnail Image
  Book (stand-alone)
  Usindikaji wa majongoo bahari kuwa chakula kiitwacho bechedema
  Mwongozo kwa wavuvi wa Visiwa vya bahari ya Pasifiki
  2021
  Also available in:

  Mwongozo huu umeundwa kwa ajili ya wavuvi wa majongoo bahari kuelewa vizuri hatua zote za kubadilisha majongoo bahari mabichi mpaka kuyakausha, ambayo huitwa ‘bechedema’. Usindikaji unajumlisha kukata, kuweka chumvi, kupika, kukausha kwa moshi na kukausha majongoo bahari juani. Bei wanayopewa wavuvi wakiuza majongoo bahari yaliokaushwa inategemea aina ya jongoo wanayouza, ukubwa wa jongoo na umakini uliotumika wakati wa usindikaji. Kuna njia nyingi ambazo majongoo bahari yanaweza kusindikwa ili kupata ubora mzuri. Mwongozo huu unaelezea njia nzuri zaidi zinazoweza kutumiwa na wavuvi kwa kutumia rasilimali zinazopatikana kirahisi vijijini kwao. Mwongozo huo una sehemu inayoelezea juu ya uvuvi wa uwajibikaji na hauhamasishi kuongeza shughuli za uvuvi.

Users also downloaded

Showing related downloaded files

No results found.